Wanaochelewesha swalah kwa ajili ya mpira

Swali: Kuna baadhi ya watu wamenukuu fatwa kutoka kwako ya kwamba umesema kuwa yule mwenye kuchelewesha swalah kwa sababu anafuatilia mpira wa miguu ya kwamba ni shirki ndogo.

Jibu: Mimi huyu nimesema hivo? Nimesema yule mwenye kuchelewesha swalah na akaitoa nje ya wakati wake pasi na udhuru wa Kishari´ah haikubaliwi. Swalah yake haikubaliwi hata kama ataswali. Lakini ni juu yake kutubu kwa Allaah. Haikidhiwi tena. Yule anayeichelewesha hailipwi tena na wala [akiiswali] haikubaliwi. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemuamrisha kulipa yule aliyepitiwa na usingizi au aliyesahau. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atayesahau swalah au usingizi ukampitia aiswali pale atapoikumbuka. Hakuna kafara yake isipokuwa hiyo.”

Ni dalili inayofahamisha kuwa yule mwenye kukusudia hailipi. Badala yake ni juu yake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kuhifadhi swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (03) http://alfawzan.af.org.sa/node/2046
  • Imechapishwa: 25/10/2016