Wanaoburuta nguo zao kwa kutumia hoja kisa cha Abu Bakr

Kuhusu ambaye anatumia hoja dhidi yetu kwa Hadiyth ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) tunamwambia kwamba hana hoja juu ya Hadiyth hiyo kwa njia mbili:

1- Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) alisema:

“Upande mmoja wa nguo yangu unashuka isipokuwa mpaka nipambane nayo.”

Haina maana kwamba yeye (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akifanya hivo kwa kukusudia. Bali ilikuwa ikimteremka. Pamoja na hivo yeye anapambana nayo.

Ama wale wanaovaa nguo zinazovuka kongo mbili za miguu na kudai kwamba eti hawafanyi hivo kwa kiburi wanakusudia kuziteremsha nguo zao. Tunawaambia kwamba wakikusudia kuziteremsha nguo zao chini ya kongo mbili za miguu pasi na kukusudia kiburi, basi wataadhibiwa kwa Moto kwa kile kilichoshuka peke yake. Na kama mnaziteremsha nguo zenu kwa kiburi basi mtaadhibiwa kwa yaliyo makubwa zaidi kuliko hayo ikiwa ni pamoja vileivile na Allaah kutowazungumzisha siku ya Qiyaamah, hatowatazameni kwa jicho la huruma, hatowatakaseni na mtakuwa na adhabu chungu.

2- Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) alitakaswa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamshuhudia kwamba yeye sio miongoni mwa wale wanaoyafanya hayo kwa majivuno. Je, hao wanaoyafanya hivo wamepata utakaso na ushuhuda huo? Lakini shaytwaan ndiye huwafanya baadhi ya watu kufuata yale maandiko ya Qur-aan na Sunnah yasiyokuwa wazi kwa lengo kuwatakasia yale wanayoyafanya. Allaah ndiye mwenye kumwongoza amkayake katika njia ilionyooka. Tunamuomba Allaah atuongoze sisi na woa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 299
  • Imechapishwa: 03/05/2020