Wanaobadilisha majina wanapoenda miji ya kikafiri

Swali 29: Ni ipi hukumu ya mwenye kuingia Marekani kwa kubadilisha jina?

Jibu: Anahesabika ni mwongo. Haifai isipokuwa kwa dharurah. Katika hali hiyo akiulizwa jina lake anaweza kusema kuwa yeye anaitwa ´Abdullaah  mwana wa ´Abdir-Rahmaan mwana wa ´Abdil-Latwiyf. Wewe ni ´Abdullaah (mja wa Allaah). Baba yako ni mwana wa ´Abdur-Rahmaan. Babu yako ni mwana wa ´Abdil-Latwiyf. Mfano wa kitu kama hichi kinafaa. Lakini usisemi kuwa jina lako ni ´Abdullaah. Bali sema kuwa wewe ni ´Abdullaah na baba yangu ni ´Abdir-Rahmaan. Mfano wa hivi inafaa. Kwa sababu sote sisi ni waja wa Allaah (´Azza wa Jall). Vinginevyo atazingatiwa kuwa ni mwongo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 70
  • Imechapishwa: 24/10/2019