Swali: Natambua kutoka kwa rafiki yangu namna alivyo na msimamo katika dini ya Allaah. Ni mtu nimemtafuta sana na namshukuru Allaah kuona nimempata. Lakini kuna tatizo; nalo ni kwamba tunafumbiana macho juu ya makosa kati yetu. Pindi ninapomzungumzisha juu ya hilo anasema kuwa mimi ni mbora kuliko yeye na kwamba lililo wajibu ni mimi kumnasihi. Shaykh! Allaah anashuhudia ya kwamba mimi nampenda mtu yule kwa ajili ya Allaah na natambua kuwa huzibadili hisia zangu na natambua kuwa ananitakia kheri. Lakini hata bado vikwazo hivo zinapatikana kati yetu. Tunaomba kutoka kwako kalima ya maelekezo kwangu mimi na kwa waislamu wengine wote juu ya maudhui hayo.

Jibu: Hapana shaka ya kwamba kupendana kwa ajili ya Allaah ni miongoni mwa matendo bora kabisa kiasi cha kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefikia kusema:

“Watu aina saba Allaah atawafunika kwenye kivuli siku ambayo hakutokuwa kivuli isipokuwa Chake… watu wawili ambao wamependana kwa ajili ya Allaah ambapo wamekusanyika kwa hilo na wakatengana kwa hilo.”

Hii ndio kamba yenye nguvu kabisa ya imani: mtu akawa anampenda mwengine na hampendi kwa jengine isipokuwa ni kwa ajili ya Allaah.

 Ni wajibu kwa kila mmoja wao – yaani wale watu wawili wanampenda kwa ajili ya Allaah – kila mmoja akamnasihi nduguye. Muumini ni kio cha ndugu yake muumini. Lakini kilicho muhimu ni vile nasaha zitavyofikishwa. Kuhusu nasaha zenyewe ni jambo la wajibu. Mtu anatakiwa kutazama wakati munasibu, sehemu munasibu na maneno munasibu. Kila mtu anakuwa kwa kiasi cha vile anavyoonelea na Allaah haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa vile inavyoweza.

Ama kunyamazia kasoro zake na yule mwengine akanyamazia kasoro zake pamoja na yale mapenzi yanayopatikana kati yao na wanachelea mapenzi haya yasije kuharibika, ni kosa. Bali kule kukosoa ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kufanya mapenzi kubakia. Kule wewe kumkosoa ndugu yako – ni mamoja ikawa kwa kile alichokufanyia wewe au amemfanyia mwengine – ni bora kuliko kunyamazia na huku bado una kinyongo. Matokeo yake kunatokea mambo na hatimaye kunatokea mfarakano.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/908
  • Imechapishwa: 08/09/2018