Wanandoa wanatakiwa kuvumiliana kwa kasoro za kila mmoja

Swali: Mimi ni mwanamke ambaye ni mtiifu kwa mume wake na nimeshikamana na maamrisho ya Allaah. Hata hivyo kamwe hatabasamu kwangu. Hatimizi majukumu yake kwangu inapokuja katika kunikatia nguo. Matokeo yake na mimi ninaacha kufanya jimaa naye. Je, napata madhambi?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) Ameamrisha wanandoa kueshi kwa wema na kila mmoja atimize wajibu wake ili mafanikio ya uhusiano wa ndoa uweze kukamilika. Mume na mke ni lazima kuvumiliana katika upungufu na uhusiano mbaya, mke atimize majukumu yake na amuombe Allaah haki zake. Hili linafanya ndoa kudumu.

Ninakuusia kuvumilia na upungufu wa mume wako na kwamba utimize majukumu yako kama mke. Mwisho – kwa idhini ya Allaah – ni wenye kusifiwa. Ikiwa mwanamke anatimiza wajibu wake, inawezekana kwa mwanaume akaanza kuona haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Makaanat-ul-Mar’ah fiyl-Islaam, uk. 634-635
  • Imechapishwa: 20/09/2020