Wanandoa kuwekeana ahadi yeyote asioe au kuolewa

Swali: Mwanamke huyu aliahidiana na mumewe asiwepo yeyote katika wao ambaye ataoa au kuolewa. Hata hivyo mume wake akaoa mwanamke mwingine na akamtaliki. Je, mwanamke huyu atimize ahadi au aolewe kama yeye alivyooa?

Jibu: Sharti hii haifai. Haijuzu kwa mume kumuwekea sharti mkewe kutoolewa na mwingine baada yake. Kwa sababu kitendo hicho kinaenda kinyume na Shari´ah. Ambaye si halali wakeze baada yake ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pekee. Mwanamke akitengana na mume wake – ni mamoja ametengana naye akiwa bado yuhai au ameshakufa – basi hapo anakuwa huru na anaweza kuolewa na amtakaye. Kumtilia sharti asiolewe na mwingine ni sharti batili na asiitimize.

Kadhalika mume akitiliwa sharti ya kutomuoa mwanamke mwingine baada yake pia ni sharti batili. Mume yuko huru ana haki ya kumuoa amtakaye hata mke wake bado yuko pamoja naye. Isipokuwa akimuwekea sharti hiyo wakati wa kuoana asioe juu yake, basi sharti hii ni sahihi kwa mujibu wa maoni yenye nguvu katika maoni ya wanachuoni. Katika hali hii akioe mwingine juu yake – ilihali alimuwekea sharti wakati wa kuoana asioe mwingine juu yake – basi ana khiyari kati ya kuifuta ndoa hiyo au kubaki pamoja naye.

Check Also

Mke anachukua pesa kutoka kwa mume kwa ajili ya haja za mustakabali

Swali: Mke anachukua pesa kutoka kwa mume wake na anasema kuwa ni kwa ajili ya …