Swali: Kuna mlinganizi ambaye yuko na alama za kheri lakini hata hivyo anamkufurisha Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na Shaykh Ibn Baaz (Rahimahumaa Allaah).  Ni ipi hukumu ya kitendo hichi na unaninasihi nini juu ya mtu huyu?

Jibu: Haya ni matendo ya Khawaarij. Khawaarij ndio ambao wanawakufurisha wanachuoni na waislamu. Haya ni matendo ya Khawaarij – Khawaarij ni kipote kinachotoka katika dini:

“Wanatoka katika dini kama ambavo mshale unatoka kwenye upinde wake.”[1]

[1] al-Bukhaariy (6/376) na Muslim (2/742).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (82) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-08-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2018