Swali: Mwanamke anaposafiri hali ya kuwa pamoja naye yuko na mwanamke mmoja tu. Katika hali hii, Mahram anakuwa si wajibu kwake?

Jibu: Hapana. Uwajibu bado uko pale pale. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Si Halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho, kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Na makusudio ya Mahram, ni yule ambaye imeharamishwa kwake kumuoa. Na makusudio hapa anaingia mume vile vile.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.info/fatwa.php?fatwa_id=639
  • Imechapishwa: 28/02/2018