Wanajua lakini wanafuata matamanio


Ni jambo linalojulikana kwamba haifai kuyafanya maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ni maalum kwa kitu fulani isipokuwa isipokuwa kwa dalili nyingine kutoka kwenye maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hayatakiwi kufanywa maalum kwa ijtihaad, uzushi na falsafa za watu. Haya ni yenye kurudishwa kwa mwenye nayo. Haya ni yenye kutambulika kupitia misingi ya Hadiyth na misingi ya tafsiri ya Qur-aan ya kwamba yaliyokuja kwa ujumla hayafanywi kuwa maalum isipokuwa kwa dalili. Yaliyokuja kwa njia ya kuenea hayafanywi kuwa maalum kwa ijtihaad za watu wenyewe. Hii ni kanuni ambayo kuna maafikiano juu yake. Ni vipi kanuni hii inaweza kufichika kwao na kusema:

“Picha kwa ala za kisasa haziingii ndani ya makatazo.”?

Kwa mujibu wa wanachuoni wa misingi maneno kama ni ya kipuuzi yasiyokuwa na maana yoyote. Kanuni za misingi zinatupilia mbali yote haya na watu hawa wanayajua haya. Lakini – Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu – wakati mwingine matamanio na kujifanya kukosea kunaweza kuwavugumiza wenye nayo sehemu ya mbali kabisa. Mtume maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila mtengeneza picha ndani ya Moto.”

na wao wanasema:

“Hapana! Picha za kisasa haziko ndani ya Moto.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 605-606
  • Imechapishwa: 05/09/2019