Wanafunzi wanataka chumba kwa ajili ya Dhuhaa´

Swali: Unajua ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali Sunnah ya Dhuhaa´ na akakokoteza kwayo. Sisi wanafunzi tulikuwa tunapendelea pia kuiswali. Je, una chochote cha kuwaambia wakuu wa masomo, mawakaala na maprofesa kutenga chumba kwa wale wanaotaka kuiswalia?

Jibu: Siwezi kuyasema haya. Nachelea akakaa kwa ajili ya kuswali halafu akaanza kucheza na marafiki zake na fursa ikampita. Wao midhali wanatafuta elimu, basi itambulike kuwa kutafuta elimu ni jambo bora kuliko kuswali swalah ya sunnah.

Pamoja na kwamba wako wanachuoni wanaosema kwamba sunnah ya Dhuhaa´ haikuwekwa katika Shari´ah. Wengine wakasema haikuwekwa katika Shari´ah kwa yule mwenye kusimama usiku na kuswali. Lakini hata hivyo maoni yenye nguvu ni kwamba sunnah ya Dhuhaa´ imesuniwa kila siku. Lau kusingelipokelewa kitu zaidi na yale aliyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba kunapambazukiwa swadaqah kwa kila kiungo miongoni mwa viungo vya mwili. Viungo viko mia tatu na sitini. Kila siku moja mtu anatakiwa kutoa swadaqah mia tatu na sitini. Lakini kusema “Subhaaan Allaah” ni swadaqah, kuamrisha mema na kukataza maovu ni swadaqah, kuondosha dhara njiani ni swadaqah. Akasema:

“Mtu anatoshelezwa na hayo Rak´ah mbili anazoswali za Dhuhaa´.”

Mtu akisahilikiwa kuziswali ndio jambo linalotakikana. Asipoweza basi wewe uko katika kheri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1337