Swali: Baadhi ya wanafunzi wanakusanya kati ya swalah ya ijumaa na swalah ya ´Aswr wanapokuwa safarini. Wanasema kuwa wao wanamfuata mmoja katika wale maimamu wane juu ya hilo. Je, kitendo chao hichi ni sahihi?

Jibu: Hatukupata katika maimamu ambao wanajuzisha jambo hili. Baadhi ya wanachuoni au mmoja katika wanachuoni ambaye kwa sasa nimemsahau jina ndiye ambaye kajuzisha. Ama kuhusu wale maimamu wane hatukupata yeyote ambaye amejuzisha kukusanya ´Aswr na swalah ya ijumaa. Lakini baadhi ya watu hupenda kwenda kinyume.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-26-10-1434.mp3
  • Imechapishwa: 21/10/2017