Wanafunzi wanakataza maovu


Swali: Kwa kuzingatia jambo la kuenea maovu wapo baadhi ya wanafunzi na walinganizi ambao wanayakemea na kusambaza fatwa za wanachuoni. Hawapinzani na mtawala. Sambamba na hilo wapo baadhi ya wanafunzi wengine ambao wanawakemea na kwamba hio ni kazi ya wanachuoni. Je, ni sahihi?

Jibu: Haya yamebainishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) pale aliposema:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayakemee kwa mkono wake.”

Haya yanawahusu wale wenye mamlaka.

“Asipoweza, afanye hivo kwa ulimi wake.”

Wale wasiokuwa na mamlaka basi wanatakiwa wawabainishie watu kwamba matendo hayo ni haramu na kwamba hayafai na kuwafahamisha. Wanatakiwa wawafahamishe kwa kuongea na hiyo ndio kazi ya walinganizi.

“Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”[1]

Huyu hana mamlaka wala elimu. Hana uwezo wa kuwabainishia watu yaliyokatazwa na kulingania kwa Allaah. Huyu inatosha kwake akakataza maovu kwa moyo wake na akajitenga mbali na watenda maasi na sehemu hiyo ya maasi.

[1] Muslim (49).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-3-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2018