Wanafunzi wa kike kwenda kusoma katika mji mwingine


Swali: Ni ipi hukumu ya wanafunzi wa kike kwenda katika vyuo vikuu ambavyo viko mbali na mji kwa takriban 75 km pamoja na kuzingatia kwamba idadi ya wanafunzi hao wa kike wanaweza kufika mpaka arobaini ndani ya basi na dereva anayewaendesha anapewa mshahara kutoka chuoni?

Jibu: Hakuna neno kwa hili ikiwa wanarudi siku hiyohiyo. Kwa mfano wanafunzi wa kike au waalimu wa kike wanaenda katika nchi nyingine 75 km au 100 km na wanarudi siku hiyohiyo na hakuna mwanaume na mwanamke kukaa faragha, kitendo hichi hakina neno. Kwa sababu hakiitwi kuwa ni ´safari` kwa mujibu wa desturi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (75) http://binothaimeen.net/content/1749
  • Imechapishwa: 25/09/2020