Wanafunzi makafiri wanaofunua nyuchi za wanawake wa Kiislamu kwa sababu ya masomo

Swali: Kati yetu kuna wanafunzi wasiokuwa waislamu katika Ahl-ul-Kitaab. Wanafunua pamoja nasi juu ya nyuchi za wanawake wa Kiislamu. Ni ipi hukumu katika hilo?

Jibu: Hukumu juu ya hilo ni kwamba hakuna neno, kama tulivotangulia kusema[1]. Lakini tunazidisha sharti ya pili; tuwe na uaminifu nao. Kwa msemo mwingine tuamini uaminifu wao. Kafiri anaweza kuaminiwa katika mambo haya. Tukiamini upande wake na haja ikapelekea kufanya hivo basi hakuna neno. Kama ambavyo muislamu pia tunatakiwa kumzidishia sharti hii. Ni waislamu wangapi hawaaminiwi juu ya nyuchi za wanawake wa Kiislamu?

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/daktari-wa-kiume-kufunua-uchi-wa-mwanamke-ili-kujua-aina-ya-maradhi-anayouguwa/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (09) http://binothaimeen.net/content/6726
  • Imechapishwa: 26/11/2020