Swali: Baadhi ya wanafunzi wanawachukua picha kwa simu watu waliokaa pembezoni mwao pasi na kuwataka wao idhini na baadhi hawataki wachukuliwe picha. Je, inajuzu?

Jibu: Hata kama wataridhia haijuzu kuchukua picha. Haijuzu kupiga picha viumbe vyenye roho. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha. Haijuzu hata kama watakubali hilo. Picha imeruhusiwa tu wakati wa dharurah. Haina neno. Ikiwa sio dharurah na lengo ni kumbukumbu na jambo jengine haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Waswiyyat-un-Nabiy http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/wasiyah%20nabi-21-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 04/07/2018