Wanafunzi kusimama kwa ajili ya mwalimu

Swali 1341: Ni ipi hukumu ya wanafunzi wa kike kumsimamia mwalimu wa kike kwa ajili ya kumuonyesha heshima?

Jibu: Haitakikani kusimama kwa ajili ya mwalimu wa kike wala wavulana kwa ajili ya mwalimu wa kiume. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba ni jambo limechukizwa sana. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hakukuwepo yeyote anayependwa zaidi kwao – yaani Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) – kuliko Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawakuwa wakisimama kwa ajili yake anapoingia kwao kutokana na wanavojua anachukia kitendo hicho.”

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule anayependa kumithiliwa na wanaume hali ya kumsimamia basi ajiandalie makazi yake Motoni.”

Hukumu ya wanawake ndio hukumu ya wanaume katika jambo hili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 544-545
  • Imechapishwa: 19/08/2019