Swali: Hivi punde kumeenea katika baadhi ya maeneo wanaume kuchanganyika na wanawake kwa njia ya kwamba mwanaume anakaa pamoja na binamu yake au pamoja na mke wa kaka yake. Wakati mwingine wanakusanyika wote katika chakula. Ni ipi nasaha yako juu ya hili?

Jibu: Kuhusu familia kukusanyika sehemu moja kwa njia ya kwamba wanawake wanakuwa upande wao na wanaume upande wao hakuna neno. Ni sawa. Maadamu hakuna fitina maalum tunayoijua kutoka kwa baadhi ya wanaume au wanawake. Katika hali hii itakatazwa. Vinginevyo asli ni kuwa inajuzu.

Ama kukusanyika [wote] kwa ajili ya kula si sahihi. Kukusanyika kwa ajili ya kula mwanamke anaweza kukaa pembezoni na mwanaume ambaye si Mahram wake wala si mume wake. Jengine ni kuwa ni vipi mwanamke atakula ilihali amefunika uso wake? Ni lazima aufunue uso wake. Kwa sababu ni jambo linalojulikana kuwa chakula kinapitishwa mdomoni. Katika hali hii ni lazima kizuizi. Kwa ajili hiyo tunaona kukataza kitendo hichi.

Kuhusu wote kukaa sehemu moja, sawa iwe kwenye kikao, sebleni na mfano wa sehemu hizo, hakuna neno ikiwa wanawake wamekaa upande wao na wanaume upande wao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (09)
  • Imechapishwa: 03/05/2020