Wanachuoni wetu wanatoa fatwa zinazohusu waislamu dunia nzima

Swali: Muulizaji huyu ni kutoka Marekani anasema: Marekani kuna mtu ambaye siku zote husema kwamba wanachuoni wa Saudi Arabia hawajui hali za waislamu huko Marekani. Basi kwa ajili hiyo hatukubali fataawaa zao na anakariri jambo hilo. Ni zipi nasaha zako juu ya hilo?

Jibu: Wanachuoni wanajua elimu aliyoteremsha Allaah na wanatoa fatwa kwa mujibu wa halali na haramu. Mambo ya halali na mambo ya haramu ni mamoja Marekani na kwenginepo. Ulimwenguni kote ni mamoja. Kitu cha haramu ni haramu kila mahali. Kitu cha halali ni halali kila mahali. Mwanachuoni anawatolea fatwa watu wa ulimwenguni kote kwa mujibu wa elimu yake yenye manufaa. Huku ni kukoseswa nusura. Mwenye kusema maneno haya ni kukoseswa nusura. Lengo lake anataka kuwatenganisha na wanachuoni wenu. Msikubali kutoka kwake maneno haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=SV_kh8eHskw
  • Imechapishwa: 03/01/2020