Wanachuoni wetu wanaishi na waislamu wa ulimwengu mzima

Wanachuoni wetu wanaozungumza katika barnamiji ”Nuur´ alaad-Darb” wanaishi na waislamu wote katika nchi zote na sio katika nchi hii  peke yake (Saudi Arabia). Wanachuoni wa nchi hii sio wa kimahali. Ni wanachuoni wa kilimwengu. Ulimwengu mzima unafaidika na elimu na fatwa zao. Ni nani ambaye hujibu yale maswali yanayotoka ulimwenguni kote? Wanachuoni! Ni kina nani ulimwengu huwapigia simu katika msimu wa haji juu ya vidokezo? Ni wanachuoni.

Kwa hivyo wanachuoni wetu ndio watambuzi zaidi wa mambo ya kisasa. Ni miongoni mwa watu wenye ufahamu mkunjufu zaidi kuyatambua mambo ya kisasa. Kwa hivyo tuishi kisasa na tuwaache wanachuoni salama.

Si nyinyi ndio ambao pale tu ambapo mtu akiwaashiria wale ambao mnawaita “walinganizi” na ”wanachuoni”, basi mnasema:

”Nyama za wanachuoni zimetiwa sumu.”?

Je, nyama za wanachuoni wakubwa ni tamu na ni dawa? Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu. Ni kwa nini kujigonga namna hii. Ni waalimu zenu. Mmesoma kupitia kwao. Pamoja na hivyo mnawachezea shere na kuwasema vibaya. Nyama zenu zimetiwa sumu na nyama zao ndio dawa? Mcheni Allaah, Mola wenu. Haifai kuwazungumza vibaya wanachuoni wa waislamu. Wanachuoni ndio warithi wa Mitume.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan bin ´Aliy al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://sahab.net/forums/showthread.php?t=385346
  • Imechapishwa: 19/01/2021