Hapa nitakuorodheshea baadhi ya vitabu vilivyothibitisha waumini kumuona Mola wao siku ya Qiyaamah Peponi. Baadhi ya wanachuoni wameviorodhesha vyenyewe katika vitabu maalum. Vivyo hivyo baadhi ya watunzi wa Ahl-us-Sunnah wamevitaja katika vitabu vyao. Vilevile waandishi wa vitabu “as-Swahiyh” na “as-Sunan” wameviwekea milango katika vitabu vyao. Wameorodhesha chini yake Hadiyth na Aathaar juu ya hayo kwa ajili ya kuwaraddi wazushi hawa ambao wanakanusha dalili za Qur-aan na Sunnah kwa kutumia akili zao. Miongoni mwa ambao wamevitungia vitabu vya kipekee ni wafuatao:

1- “Kitaab-ur-Ru´yah” cha Imaam ad-Daaraqutwniy.

2- Imaam Abu Na´ym.

3- “Taswdiyq bin-Nadhwar” cha Imaam al-Aajurriy.

Kuhusu watunzi waliotaja Hadiyth kuhusu kuonekana Allaah katika vitabu vyao miongoni mwao ni wafuatao:

1- Imaam Ibn Battwah.

2- al-Laalakaa´iy katika “Sharh Usuul I´tiqaad Ahl-is-Sunnah” katika mjaladi wa pili ukurasa wa 454-533.

3- Ibn Hishaam.

4- ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal katika kitabu chake “as-Sunnah”.

5- Imaam ad-Daarimiy katika radd yake kwa Jahmiyyah chini ya mlango “ar-Ru´yah”.

6- Hanbal bin Ishaaq.

7- al-Khallaal.

8- at-Twabaraaniy.

9- Ibn Mandah katika kitabu chake “al-Iymaan” na ametaja kuhusu hilo kipengele kirefu.

10- Ibn Mandah katika radd yake kwa Jahmiyyah ambaye ameanza hilo mwanzoni mwa kitabu.

11- Ibn Abiy ´Aaswim katika “as-Sunnah” ambapo amesema katika ukurasa 96: “Mlango unaozungumzia yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu namna tutakavyomuona Mola wetu huko Aakhirah.

12- Ibn-ul-Qayyim katika “Haadi al-Arwaah”.

Miongoni mwa waliotunga vitabu “as-Swahiyh” ni wafuatao:

1- Imaam al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake katika Kitaab-ut-Tawhiyd chini ya mlango: “Ujuwhun yauma-idhin naadhwirah ilaa Rabbihaa naadhwirah”.

2- Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake katika kitabu “al-Iymaan” mlango “Ma´rifat-ut-Twariyq Ru´yah”.

Miongoni mwa waliotunga vitabu “as-Sunan” ni wafuatao:

1- Imaam Abu Daawuud katika kitabu chake “as-Sunnah” (05/97). Mlango: “Ru´yah”.

2- Imaam Ibn Maajah katika utangulizi wake: “Mlango: “Fiymaa ankarat al-Jahmiyyah” na akaanza kutaja Hadiyth inayozungumzia Kuonekana.

Kuna wanachuoni wengine wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah mbali na hawa. Tumewataja hao ili apate kurejea yule anayetaka.

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika kila zama na mahala hawawaachi wazushi hawa na utatizi na kutaka kwao kuwapaka waislamu mchanga wa machoni. Wanafichua upindaji wao na wanabainisha makosa yao kwa mujibu wa yale yaliyokuja katika Qur-aan, Sunnah na maneno ya Maswahabah na Taabi´uun miongoni mwa wale watu waliokuwa katika karne bora ambao wameshuhudiliwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ni bora. Imepokelewa katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na wengineo ya kwamba:

“Watu bora ni wa karne yangu. Kisha wataofuata. Kisha watakaofuata… “

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 141-143
  • Imechapishwa: 14/01/2017