Kabla ya siku kadhaa nimekutana na mwamali wa ISIS. Anauliza ni vipi tunaweza kutahadharisha juu ya IS na dola ya Kiislamu inayoongozwa na Abu Bakr al-Baghdaadiy ilihali wanasapotiwa na wanachuoni wakubwa ´Iraaq na mwanachuoni mkubwa Misri.

Nikamwambia, kuhusiana na wanachuoni wakubwa wa ´Iraaq wametokomezwa na Saddaam, halafu Raafidhwah, halafu al-Qaa´idah kisha ISIS. Nina mawasiliano mazuri na ndugu wa huko ´Iraaq na najua kilichopitika. Maimamu wa misikiti mingi wameuawa na kuchinjwa; tokea wakati wa Saddaam mpaka hii leo. Wametokomezwa kwa sababu ya watu wa fitina, watu wa utata na watu wa matamanio. Ni wanachuoni wepi wa ´Iraaq unaokusudia?

Halafu nikamuuliza ni mwanachuoni yupi unayekusudia [Misri]. Akanambia ni Muhammad Twarhuuniy. Anawasapoti naye ndiye mwanachuoni mkubwa kabisa hii leo ulimwenguni.

Nikamuuliza kama yeye hampendi muheshimu Muftiy, Shaykh al-Fawzaan, Shaykh al-Luhaydaan na wanachuoni wengine wakubwa. Hapana, yeye ni mjuzi zaidi kuliko hawa, ndivyo alivyosema.

Tazama mjinga huyu namna alivyoambatana na watu kulivyomfanya akafikia mpaka huu; kuambatana na watu na kutokuwa na uelewa.

Nikamuuliza kama ameshakutana naye. Hapana, nimepata elimu yake kwenye intaneti, ndivyo alivyosema.

Mtu huyu mnamjua. Alipewa mtihani wa Takfiyr na akatimuliwa kwenda mji wake. Halafu ndipo akaanza kueneza sumu yake. Hivi sasa anawasapoti ISIS. Saudi Arabia ilimfanyia huduma hakuitolea shukurani hata kidogo. Nchi ilimfundisha na kumsomesha. Hatimaye akawashukuru kwa kuwafanyia ubaya waliomfanyia wema. Tazama namna ambavyo watu wanafikia katika mpaka kama huu kwa sababu ya kuwapenda watu.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: t.co/YFszT1eB6o
  • Imechapishwa: 06/11/2016