Wanachuoni wa Takfiyriyyuun na Salafiyyuun


Ni masikitiko makubwa mtoto wako akauawa kwa mfumo kama huu; amejilipua, kulipua wengine au kulipua sehemu fulani. Ni hasara kubwa. Sababu ni kutofuata nasaha. Sisi tunatoa nasaha kwa sababu dini ni kupeana nasaha. Hii ni amana. Chungeni nafsi zenu, wana wenu, majumba yenu, misikiti yenu na wanawake wenu. Kama jinsi kuna wanaume ambao ni Takfiyriyyuun kadhalika kuna wanawake ambao ni Takfiyriyyaat ambao wanakufurisha jamii na wanawakufurisha watu. Mwenendo wa Takfiyriyyuun unajulikana. Wanapatikana wanawake pia wenye mwenendo kama huu uliopinda. Sisi mizani yetu ni Qur-aan na Sunnah. Wao mizani yao ni vurugu, fujo na yale aliyosema Takfiyriy fulani. Sisi wanachuoni wetu ni wa wazi; Shaykh Ibn Baaz, Shaykh Ibn ´Uthaymiyn, Shaykh Muqbil, Shaykh al-Albaaniy, Shaykh al-Fawzaan, Shaykh al-´Abbaad, Shaykh ´Ubayd al-Jaabiriy, Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy na wanachuoni mfano wa hawa. Tunawaambia: tuleteeni fatwa ya mmoja katika wanachuoni hawa ambaye anajuzisha kulipua majumba, magari, mashirika au nyumba za serikali? Leteni fatwa ya mwanachuoni mmoja katika hawa anayejuzisha matendo haya? Uhakika wa mambo ni kwamba wao wanaharamisha mambo haya. Sisi tumeshikamana na wanachuoni wetu. Wanachuoni wetu wanaonelea kuwa haya ni matendo ya jinai na kueneza ufisadi baada ya kutengemaa kwake. Haya ni tofauiti na wale wanaowafuata [Takfiyriyyuun]. Wanawajuzishia kulipua, kuharibu na kuangamiza. Hawajali atayekufa. Hali ilivyo leo inatosha kuwa ni ushahidi. Hali ya Khawaarij ilivyo leo inatosha kuwa ni ushahidi mkubwa. Hali yao leo ilivyo Syria, Misri, Yemen, Tunisa, Libya, Marocco, siku za nyuma Saudi Arabia na miji mingine ndio uhakika wa mambo yao. Upande mwingine wanachuoni waheshimiwa wanaharamisha mambo haya na wanasisitiza kujifunza elimu,

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ath-Thabaat ´alaa as-Swiraat al-Mustaqiym yakuun bil-´Ilm http://olamayemen.com/Dars-9998
  • Imechapishwa: 04/05/2018