Ambaye atasoma historia basi ataona kuwa wanachuoni ndio wako imara zaidi kuliko wafanya ´ibaadah. Kwa sababu wanatenda kwa elimu na umaizi. Hivo ndivo walivyosifiwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Katika mnasaba wa mambo yenye kutatiza na mambo yenye shubuha wanachuoni wanatenda kwa mujibu wa elimu na umaizi. Kwa ajili hiyo ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaingiza pia wao juu ya nafsi yake pindi Allaah alipomwamrisha kusema:

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata. Utakasifu ni wa Allaah na mimi si miongoni mwa washirikina!”[1]

Ummah huu ulidhoofika pale ambapo watu walipoanza kuifanyia kazi dini kwa ujinga. Hivo ndivo walivofanya Khawaarij na Ahl-ul-Bid´ah wengine wanaokwenda kinyume na Sunnah. Walimili katika matendo mema, lakini walifanya hayo kinyume na Sunnah na kinyume na njia ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Matokeo yake wakawa wanasemwa vibaya na kila mtu. Kwa hiyo kutokana na historia wanachuoni ndio wabora, wenye akili zaidi, wajuzi zaidi na ndio wenye athari kubwa juu ya Ummah huu.

Kulipokuja fitina ya kuumbwa kwa Qur-aan na Imaam Ahmad akasema aliyoyasema, kuna mmoja katika maimamu aliyeulizwa – sijui kama alikuwa Ishaaq au mwingine – ni nani mjuzi zaidi katika watu ambapo akajibu kwa kusema:

“Ahmad.”

Alisema hivo kwa sababu ya kuashiria kwamba kuwa kwake imara katika fitina kulikuwa kumetokana na ubobeaji wa elimu yake juu ya Tawhiyd na Sunnah.

[1] 12:108

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Fadhwl-ul-´Ilm wa Ahlihi wa Swifatuhum http://saleh.af.org.sa/sites/default/files/101.mp3
  • Imechapishwa: 05/07/2020