Swali: Wale wanachuoni ambao wanawaona watu wa kawaida wanafanya shirki na wanatufu kuyazunguka makaburi, wanayachinjia, wanayawekea nadhiri na wakati huohuo wananyamaza – je, wakufurishwe?

Jibu: Hapana, wasikufurishwe. Ni wenye kupaka mafuta. Ni tendo la jinai kwa kunyamaza. Hawakufuru isipokuwa pale ambapo wataona kuwa mtu huyu ni mwenye kupatia kwa kitendo chake hichi. Wakiona kuwa ni wenye kupatia na wako katika usawa ndipo wanakufuru.

Muulizaji: Lakini wanajua kuwa matendo haya ni shirki ya wazi?

Ibn Baaz: Hata kama. Hawakufuru. Kuna uwezekano ikawa ni kupakana mafuta na ni kuchukulia wepesi, mambo yanayofanywa na baadhi ya wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 43
  • Imechapishwa: 18/06/2019