Wanabaki nje ya msikiti wakisubiri darsa mpaka kumalizwe kuswaliwa

Swali: Unasemaje juu ya wale wenye kusimama pembezoni mwa msikiti wakati watu wako wanaswali katika msikiti huu katika usiku kama huu mpaka swalah imalizike kisha wanaingia msikitini ili kuhudhuria muhadhara huu uliobarikiwa. Je, matendo haya wanayofanya ni sahihi au lililo bora ni wao kuingia ndani ya swalah pamoja na imamu na kwao iwe ni Naafilah?

Jibu: Matendo yao ni sahihi. Kwa msemo mwingine ni kwamba hawapati dhambi kwa kufanya hivo. Lakini lililo bora ni wao waingie msikitini na waswali pamoja na waislamu wenzao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu watu wawili aliowaona wameacha kuswali swalah ya Fajr katika msikiti wa al-Khayf Minaa ambapo akawaendea na wakaanza kutetemeka kutokana na haiba ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akasema:

“Ni kipi kilichokuzuieni kuswali na wengine?” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Tumeswali majumbani mwetu.” Akasema: “Mkiswali majumbani mwenu kisha mkaja msikitini na mkakuta wanaswali mkusanyiko, basi mswali pamoja nao. Hakika kwenu – yaani swalah hiyo ya pili – itakuwa ni Naafilah.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1482
  • Imechapishwa: 30/01/2020