Wamche Allaah waume wanaosema “Tunajua kuoa hatujui kuacha”

Swali: Afanye nini mwanamke aliyemuomba mume wake talaka ambapo akakataa?

Jibu: Akimuomba talaka kwa sababu inayokubalika katika Shari´ah basi hatakiwi kukataa. Bali ni lazima kwake kumcha Allaah na aombe mahari yake na haki yake. Mwanamke akikataa kumpa haki yake basi hana haki ya talaka. Ni lazima amrudishie haki yake kikamilifu. Akikataa basi waende mahakamani na waitazame kesi hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3551/%D9%85%D8%A7%D8%B0%D8%A7-%D8%AA%D8%B9%D9%85%D9%84-%D9%85%D9%86-%D9%8A%D8%A7%D8%A8%D9%89-%D8%B2%D9%88%D8%AC%D9%87%D8%A7-%D8%AA%D8%B7%D9%84%D9%8A%D9%82%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 23/02/2020