Walioko nje ya msikiti kujiunga pamoja na imamu


Swali: Ni kipi kidhibiti juu ya swalah ya maamuma pamoja na imamu katika hali ya kutokuweko uwezekano wa kumuona imamu kama kwa mfano wako kwa juu?

Jibu: Ikiwa anasikia sauti, Takbiyr au anawaona baadhi ya maamuma hakuna neno. Ama akiwa nje ya msikiti haifai. Isipokuwa ikiwa kama safu zimekamatana. Kwa mfano msikiti umejaa na safu zikawa zimekamatana mpaka barabarani ni sawa. Ama ikiwa kati yake yeye na msikiti kuna njia inayopita magari, basi asimfuate imamu. Vivyo hivyo akiwa katika nyumba nyingine. Ni lazima waweko msikitini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 30/03/2018