Swali: Je, wale wanaolingania katika kuwafanyia uasi watawala wa Kiislamu, maandamano na migomo wanaingia katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) “walinganizi katika milango ya Motoni”?

Jibu: Bila ya shaka. Wale wenye kutaka kuwaletea fitina waislamu, migomo kwa watawala na kutenganisha umoja ni walinganizi katika milango ya Motoni. Hili halina shaka. Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameamrisha umoja, kusikiliza na kutii. Hii ndio sababu ya nusura kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Migawanyiko, usaliti, mfarakano katika umoja wa waislamu na kukosekana utiifu na mtawala wa Kiislamu yanaleta fitina na kufungua njia ya fitina na shari. Watu kama hawa wasisikizwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Tahdhiyr min Du´aat-is-Suu’
  • Imechapishwa: 05/09/2020