Kunyamaza na huku wanasemwa vibaya Maswahabah, ´Aqiydah inaharibiwa, Uislamu na Ahl-us-Sunnah wanapigwa vita na wewe huku umekaa kimya, huu ni woga na ni khiyana na unyenyekevu wa batili.

Kuna ambao wanakosea na wanawatatiza wajinga na wanawaambia kuwa mambo haya ni kusengenya, watu hawa hawana shughuli nyingine isipokuwa kuwasema watu. Ni sahihi wataangamia ikiwa kweli kama hawana shughuli nyingine isipokuwa kuwasema watu na ni ubaya ulioje wa kitendo hichi. Lakini ikiwa wamekusudia nasaha kwa ajili ya Allaah, basi ni katika matendo mema.

Tusemeje juu ya Salaf ambao wametahadharisha Jahmiyyah, Mu´tazilah, Khawaarij, Rawaafidhw, Murji-ah, kila mtu wa Bid´ah, maasi, pombe, zinaa, machafu na wengine kwa kuwataja majina? Kwa mujibu wa watu hawa kufanya hivi ni kupetuka mipaka [Ghuluw]. Mashaa Allaah! Huyu hana shughuli nyingine isipokuwa kuwakosoa watu! Huku ni kutoa nasaha na sio kuwakosoa watu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/205-206)
  • Imechapishwa: 19/05/2015