Swali: Pindi tunapotahadharisha vitabu vilivyoandikwa na wenye ´Aqiydah iliyopidwa, wanatumia hoja kwa kusema kwamba ´Allaamah Ibn Baaz alimshufaia miaka arobaini iliyopita wakati alipotaka kuuawa, na kwamba Idhaa´at-ul-Qur-aan iligawa tafsiri ya Qur-aan yake na kwamba vitabu vyake vilikuwa vikigawanywa kwenye madarasa. Vipi tutaraddi hili?

Jibu: Hii sio hoja. Ikiwa vina makosa, makosa ni yenye kurudishwa. Hao ambao unasema kuwa walimtetea walikuwa hawajui yaliyomo. Kuhusiana na kwamba Ibn Baaz alimshufaia, ilikuwa ni uombezi katika jambo zuri; muislamu ni mwenye kuzuia mauaji. Ni uombezi katika jambo zuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Waswiyyat-un-Nabiy http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/wasiyah%20nabi-21-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 15/07/2018