Walii wa mwanamke ambaye kasilimu


Swali: Kuna ndugu yetu mmoja anataka kumuoa mwanamke ambaye ndio punde katoka kuingia katika Uislamu na hana Mahram. Ni vipi ataweza kumuoa mwanamke kama huyu na ni nani walii wake?

Jibu: Ikiwa yuko katika nchi ya Kiislamu, basi aende kwa Qaadhiy wa kidini; atamfungisha ndoa. Ikiwa yuko katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu, aende kwa mudiri wa kituo moja wapo cha Kiislamu. Mudiri wa kituo moja wapo cha Kiislamu ndiye anayechukua nafasi ya Qaadhiy. Yeye ndiye atamuozesha ikiwa hana walii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (79) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-9-2-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 09/03/2018