Walii Ni Bora Kuliko Mtume?


Swali: Ni vipi wataraddiwa Suufiyyah ambao wanatumia kisa cha Muusa pamoja na Khidhr ya kwamba walii ni bora kuliko Mtume kwa kuwa Muusa alijifunza kutoka kwa Khidhr ambaye alikuwa ni walii?

Jibu: Hakujifunza moja kwa moja. Pindi alipoulizwa:

“Ni nani mjuzi zaidi wa watu?”

Akajibu:

“Ni mimi.”

Ndipo Allaah akataka kumbainishia kuwa amekosea katika hili na kwamba kila kwenye mjuzi kuna mjuzi zaidi. Hata kama mtu atakuwa ni msomi aliyebobea kabisa kunaweza kuwa ambaye ni mjuzi zaidi kuliko yeye katika baadhi ya mambo. Allaah alitaka kumfunza Muusa ya kwamba si sawa kusema kuwa yeye ndiye kiumbe aliye mjuzi zaidi. Kuna ambaye ni mjuzi zaidi kuliko yeye katika baadhi ya mambo. Muusa hakujifunza Ujumbe kutoka kwa Khidhr. Alijifunza baadhi ya mambo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (13) http://alfawzan.af.org.sa/node/2056
  • Imechapishwa: 09/04/2017