Swali: Kila ambaye ni walii na kukapitika mambo yasiyokuwa ya kawaida kwenye mikono yake ataingia Peponi kama alivyosema (Ta´ala):

لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا

”Watapata bishara katika uhai wa dunia.”?

Jibu: Akiwa katika Uislamu ataingia Peponi. Kuhusu akifa katika usiokuwa Uislamu… Mtu hakukingwa na kukosea. Bi maana anaweza kupinda, anaweza kupotea n.k. Akifa katika usiokuwa Uislamu anakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Kinachozingatiwa ni namna mtu anavyomalizia.

Lakini mara nyingi ni kwamba yule ambaye Allaah atamkinga na akawa miongoni mwa mawalii wa Allaah humhifadhi na humfanya akamaliza kwa wema. Vinginevyo walii hakukingwa na kukosea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2044
  • Imechapishwa: 08/10/2016