Swali: Kuna baadhi ya ndugu zetu Salafiyyuun ambao wanakaa na Ahl-ul-Ahwaa´.

Jibu: Nitakutajieni baadhi ya mifano. Haya yalitokea kwa Ibn ´Aqiyl, al-Bayhaqiy, Harawiy na wengine wengi katika historia ya Kiislamu. Wengi walidanganyika na nafsi zao na wakakaa na Ahl-ul-Ahwaa´. Matokeo yake wakapotea. Katika msingi huu kuna mazingatio na mawaidha mengi kabisa kutoka kwa watu ambao walikuwa wakiwafuata Salafiyyuun. Kule kukaa nao, kuchanganyika nao na kusoma vitabu vya Ahl-ul-Baatwil wakawa wamepotea.

Nasaha kwa watu hawa wafaidike kutoka kwa ndugu zao na kabla ya hilo wafaidike kutoka katika mfumo huu tukufu ambao unakokoteza juu ya usalama na mtu kuikoa nafsi yake. Hakuna kitu kinacholingana na usalama.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah http://rabee.net/ar/questions.php?cat=29&id=273
  • Imechapishwa: 28/04/2018