Walianza kujitokeza Khawaarij au Raafidhwah?

Swali: Ni pote lipi lililotangulia kujitokeza kati ya Khawaarij na Raafidhwah?

Jibu: Udhahiri – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni Khawaarij. Hawa ndio ambao walimuua ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na wakamfanyia uasi ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Halafu baada ya hapo ndipo wakajitokeza Shiy´ah ambao ni wafuasi wa Ibn Sabaa´. Wanakaribiana.

´Abdullaah bin Sabaa´ ndio muasisi wa Shiy´ah. Alikuwa ni mnafiki na zandiki ambaye alidai kumpenda ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah (02)
  • Imechapishwa: 01/05/2020