Wale wanaoswali kwa kuachia mikono wana dalili yoyote?

Swali 19: Je, wana dalili wale wanaoswali kwa kuteremsha mikono chini?

Jibu: Wale wanaoteremsha wana vituko na vitakuro. Kuhusu dalili hawana dalili. Lakini wamesema baadhi yao kwamba wako waliokuwa wakiswali wakiwa na sanamu ambapo wanaiweka mikono yao juu ya masanamu. Wanawajengea dhana mbaya Maswahabah. Haya ni maneno ya ujinga. Kipindi ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha kuteremsha mikono ndipo masanamu yakaanguka. Yako maoni yanayosema hivo.

Maoni ya pili yanasema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliuweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto ndani ya swalah na wakati mwingine akaachia mikono. Kwa hivyo wanasema matendo mawili yote yanajuzu. Lakini haikuthibiti eti Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliachia mikono yake. Hayo tumeyataja katika “Riyaadhw-ul-Jannah fiyr-Radd ´alaa ´adaa’ as-Sunnah”. Jambo hilo halikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Naona kuwa kitendo hicho ni cha Bid´ah. Hata hivyo sio Bid´ah inayomtoa mtu katika dini. Yule anayeswali kwa kuachia mikono sio kama mkomunisti, Ba´thiy au mnaswara.

Ahl-us-Sunnah wana uadilifu. Kuhusu Shiy´ah mnajua nini wanachosema? Wanasema kuwa Wahhaabiyyah wana madhara zaidi juu ya Uislamu kuliko wakomunisti. Hapana. Sisi tunasema kuwa wakomunisti wana madhara zaidi juu ya Uislamu kuliko Shiy´ah. Ba´thiyyah wana madhara zaidi juu ya Uislamu kuliko Shiy´ah. Manaswara wana madhara zaidi juu ya Uislamu kuliko Shiy´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 61
  • Imechapishwa: 06/10/2019