Wala Haya Sio Maneno Ya Ahl-ul-Bid´ah, Ni Maneno Ya Makafiri


Swali: Anayesema kuwa mawalii wa Allaah wana karama kama walizonazo Mitume mpaka kuwafufua wafu…

Jibu: Mitume wana miujiza isiyoweza yeyote isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah ameifanya miujiza kuwa ni maalum kwa Mitume.

Kuhusu mawalii hawana miujiza. Wao hufanya tu mambo yasiyokuwa ya kawaida pasi na miujiza.

Swali: Je, haya ni maneno ya Ahl-us-Sunnah au ni maneno ya Ahl-ul-Bid´ah?

Jibu: Wala Ahl-ul-Bid´ah hawana maneno haya. Haya ni maneno ya makafiri. Hakuna yeyote anaweza kuwahuisha wafu isipokuwa Allaah pekee na yule ambaye Allaah amemuwezesha kufanya hivo. Mmoja wao ni al-Masiyh (´alayhis-Salaam). Hii ni miujiza ya al-Masiyh. Miujiza ya Mitume haiwi kwa wengine. Hakuna yeyote anaweza kuwahuisha wafu isipokuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) na yule ambaye Allaah humjaalia akafanya miujiza kama al-Masiyh (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). Inamuhusu yeye tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (02) http://alfawzan.af.org.sa/node/2045
  • Imechapishwa: 12/10/2016