Swali: Mayahudi na wakristo waliopo hii leo ni Ahl-ul-Kitaab?

Jibu: Mimi naona kuwa ni Ahl-ul-Kitaab. Midhali wanaamini dini ya Ahl-ul-Kitaab au wanajinasibisha na dini ya Ahl-ul-Kitaab basi wao ni Ahl-ul-Kitaab. Kwa sababu Allaah ametaja katika “al-Maaidah”:

وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ

“… na chakula cha wale Ahl-ul-Kitaab ni halali kwenu.”[1]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

licha ya kuwa katika Suurah hiyohiyo ya “al-Maaidah” amesema:

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ

“Hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni al-Masiyh mwana wa Maryam.”[2]

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ

”Hakika wamekufuru wale waliosema: ”Hakika Allaah ni watatu wa utatu.”[3]

Amewakufurisha na wakati huohuo akahalalisha chakula chao.

Hata pamoja na uharamishwaji ni jambo lililokuwa tokea wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Wakisema kuwa wameikataa dini ya Ahl-ul-Kitaab na kwamba hawaitambui na hatuingii ndani ya Uislamu na tunataka ukomunisti kwa sababu wanaona kuwa hakuna mungu wala mola, hawa jambo lao liko wazi. Lakini watu wanaamini dini ya ukristo, wanaswali kwenye makanisa na wanawarehemu maiti wao na wanasherehekea sikukuu zao – ingawa ni dini za kikafiri lakini wanaona kuwa zinafaa kwao – wana hukumu moja kama ya Ahl-ul-Kitaab.

[1] 05:05

[2] 17:05

[3] 05:73

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (94) http://binothaimeen.net/content/3888
  • Imechapishwa: 15/01/2020