Wakimbizi wanafupisha swalah miji ya uzunguni


Swali: Kuna wakimbizi huku kwetu (Sweden) wanaomba visa kutoka serikali na wanabaki huku kwa miaka mingi na wanafanya kazi na kufupisha swalah. Pindi tunapowauliza wanasema kuwa ni wasafiri. Je, hii inahesabika kuwa ni safiri kwa kuzingatia ya kwamba wanajaribu kupata visa kutoka katika nchi hii?

Jibu: Kwa upande wa kujumuisha na kufupisha haijuzu kwako kufanya hivo. Haijuzu kwa mtu kujumuisha na kufupisha akinuia kukaa katika mji zaidi ya siku nne. Akinuia kukaa katika mji zaidi ya siku nne, katika hali hii haijuzu kwake kujumuisha na kufupisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah (01)
  • Imechapishwa: 06/09/2020