Wakazi wa Ulaya wanataabika kupata kazi isiyo na kasoro

Swali: Sisi ni vijana tunaishi Ufaransa na tunafuata mfumo wa Salaf-us-Swaalih. Tumelazimika kutafuta riziki na hatupati kazi iliyosalimika na mambo yanayoenda kinyume na Shari´ah. Unatunasihi vipi?

Jibu: Ni juu yenu kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kiasi na uwezo wenu:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُم

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Mkimcha Allaah vile na mnavyoweza basi Allaah hatokukalifisheni zaidi na vile mnavyoweza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (37) http://alfawzan.af.org.sa/node/2148
  • Imechapishwa: 13/07/2020