Swali 344: Ni wakati upi wa mwisho mtu anaweza kuiwahi swalah ya Witr?

Jibu: Ni ule wakati wa mwisho katika usiku kabla ya kuchomoza kwa alfajiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya usiku ni [Rak´ah] mbili mbili. Atapochelea mmoja wenu kuingiliwa naa Subh basi aswali Rak´ah moja awitirishe kile alichokiswali.”

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 132
  • Imechapishwa: 03/09/2019