Swali: Katika mji wetu kipindi kunanyesha sana kunakuwa taka za mafuriko mengi. Ni jambo lenye kujulikana kuwa yanakuwa na maji machafu ya kutoka vyooni. Ni lazima kwa mtu kuosha miguu yake ikiwa atakanyaga mguu wake ndani ya maji hayo?

Jibu: Hapana. Asioshe. Kwa jumla ni kwamba siku zote kunakuwa uchafu na hadathi kwenye barabara. Hata hivyo Allaah hakutulazimisha kuosha miguu yetu kila tunapotembelea kwenye barabara. Hali kadhalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa ardhi ni safi. Ukikanyaga kitu najisi halafu ukakisafisha kwa ardhi basi inaiondosha najisi hiyo. Dini ni sahali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%208%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017