Swali: Kuna mtu amechukua na kuitakidi fikira za Khawaarij. Anasema kuwa hilo halimdhuru kwa sababu hakumweleza yeyote na wala hakulitendea kazi. Anatumia hoja kwa Hadiyth inayosema:

“Allaah ameusamehe Ummah wangu kwa yale yanayohadithiwa na nafsi zao.”

Je, anayosema ni sahihi?

Jibu: Hapana, si sahihi. Usisome fikira za Khawaarij isipokuwa ikiwa kama unataka kuwaraddi na kutahadharisha mfumo wao. Mantiki ya kusema kuwa eti ujifunze nayo na usiyatendee kazi si sahihi. Atadanganyika kwa njia hiyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017