Wakati ambapo Ibn ´Umar na Ibn ´Abbaas walitoa Zakaat-ul-Fitwr

810 – Nilimsikia baba yangu akisema:

“Ibn Umar alitoa Zakaat-ul-Fitwr siku moja au mbili kabla.”

811 – Mara nyingi sana nilimwona baba yangu akitoa Zakaat-ul-Fitwr siku moja kabla.

812 – Mus´ab ametuhadithia: Maalik amenihadithia, kutoka kwa Nafiy’ ambaye amenihadithia:

“Ibn Umar alikuwa akiwaagizia Zakaat-ul-Fitwr watu wanaoisambaza siku moja, mbili au tatu kabla ya ´Iyd-ul-Fitwr.”

813 – Baba yangu amenihadithia: Hushaym amenihadithia: Hajjaaj ametukhabarisha, kutoka kwa ‘Atwaa’ ambaye ameeleza kwamba:

“Ibn ´Abbaas alitoa Zakaat-ul-Fitwr kabla ya kwenda kuswali siku ya ´Iyd.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaail-ul-Imaam Ahmad (2/589)
  • Imechapishwa: 01/05/2022