Swali: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa Khatwiyb kuja mapema siku ya ijumaa ili aweze kupata thawabu zilizotajwa katika Hadiyth:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amelinganisha yule mwenye kuja katika swalah ya ijumaa mapema ni kama ambaye amechinja ngamia, kisha kama ambaye amechinja ng´ombe, kisha kama ambaye amechinja kondoo mpaka alipotaja kuku.”

au anatakiwa aje kabla ya Khutbah?

Jibu: Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba alikuwa akija wakati wa Khutbah. Aanze moja kwa moja Khutbah. Hahitajii kuswali Tahiyyat-ul-Masjid.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (91) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-22-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 12/08/2018