Wajibu wetu wakati wa kutokea janga

Swali: Unajua yale magonjwa yaliyowapata waislamu kusini mwa nchi. Ni zipi nasaha zako juu ya hilo? Ni lipi jukumu la walinganizi katika mfano wa hali kama hii?

Jibu: Ni lazima kwa waislamu kumnyenyekea Allaah, waelekee Kwake, wanasihike na wachukue mazingatio, wasubiri, watarajie malipo kutoka kwa Allaah na watubie kwa Allaah (´Azza wa Jall) kutokamana na kila dhambi na maasi. Amesema (Ta´ala):

وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ

“Haukupateni katika msiba wowote basi ni kwa sababu ya yale yaliyochuma mikono yenu na anasamehe mengi.”[1]

Mtu anatakiwa kuzingatia na achukue masomo na mazingatio. Aidha atubie kwa Allaah (´Azza wa Jall) na afanye matendo mema kwa wingi.

[1] 42:30

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 22/01/2022