Tusidanganyike na mtu wa Bid´ah hata kama atakuwa ni mtu wa dini na ´ibaadah na kulingania katika Uislamu. Tayari nimeshabainisha na kuliweka wazi suala hili. Lakini hata hivyo nakariri kutokana na haja yake na kwa sababu wengi wanaojinasibisha na kulingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall) wana elimu chache juu ya hilo hii leo. Shaykh na ´Allaamah ´Abdul-Latwiyf bin ´Abdir-Rahmaan bin Hasan bin Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) ameandika katika barua yake kwenda kwa Ibn ´Ajlaan ambaye alipendekezwa na baadhi ya wanajeshi wa kituruki na kutaja wema wao na mfano wa hayo:

“Unadai vilevile kuwa maaskari wakubwa ni wema na mfano wa haya. Hizi ni njama za kishaytwaan – Allaah akukinge na shari na joto lake. Hata kama tutasema kuwa ni wema hata Ibn ´Arabiy, Ibn Sabu´ayn na Ibn Faaridh vilevile wanaita katika ´ibaadah, swadaqah, kujiepisha na anasa na kuipa kisogo dunia. Pamoja na hivyo wao ndio makafiri wakubwa wa ulimwenguni na angalau kwa uchache washirikina wakubwa wa ulimwenguni.” Majmuu´at-ur-Rasaa-il wal-Masaa-il an-Najdiyyah.

Mambo haya hayatakasi kutokuwapenda Ahl-ul-Bid´ah kwa sababu wao ni Ahl-ul-Bid´ah. Kwa sababu hii tu ni wajibu kwetu kujitenga nao mbali, kujitenga nao, kuwatupilia mbali na kuwaponda waziwazi, kubainisha makosa na kutahadharisha nao.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 67-68
  • Imechapishwa: 09/08/2020