Wajibu wetu juu ya watenda maasi


Swali: Hakika moyo wangu umeyazingatia sana yale niliyosikia kwako kuhusu hali za watu hii leo na nimesikia mengi kuhusu hayo. Swali langu ni vipi tutataamiliana na watu hawa? Je, wanafunzi wawatembelee, kuwaelekeza na kuwazawadia kanda ndani ya nyukumbi hizi za mapumziko au tufanye vipi ili dhimmah zetu zitakasike au tupate udhuru mbele ya Allaah (Ta´ala)?

Jibu: Udhahiri ni kwamba mtu huyu ameandika swali hili wakati sisi tulipokuwa tunazungumzia yale ambayo ni wajibu kwetu juu ya ndugu hawa. Tulibainisha kuwa lililo la wajibu ni sisi kuwanasihi. Ikiwa hatukuweza kwa sababu ima ya kuona haya, kushindwa au kuogopa basi tuwafikishie wale wanaoweza kuwanasihi au kuwakataza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (39) http://binothaimeen.net/content/883
  • Imechapishwa: 15/08/2018