Wajibu wa wanafunzi juu ya wengine

Wanafunzi wana wajibu aina mbili:

1 – Kwake mwenyewe.

2 – Kwa watu wengine.

Wanafunzi wanatakiwa kuwafunza, kuwaelekeza, kulingania katika dini ya Allaah na kuwabainishia haki iliyokuja ndani ya Qur-aan na Sunnah waliyojifunza kutoka kwa waalimu zao, walioisoma ndani ya vitabu na kwenye kaseti kutoka kwa watu waaminifu.

Hapana shaka kwamba kueneza elimu ni sababu ya kutekeleza kumtii Allaah. Pindi mtu anapowaendea watu na kuwatolea kalima, baadaye watu wakatawanyika na wamefahamu kile alichokisema. Kisha wanatendea kazi yale aliyoyasema juu ya nafsi zao wenyewe na kwa wengine. Hili ni jambo linalojulikana.

Juu ya mustakabali mtu anapasa awe siriazi na mwenye kujitahidi na kutathmini yale aliyoyafanyia upungufu katika mwaka uliopita na arekebishe yale aliyokosea mwaka uliopita. Mtu akijizoweza uvivu basi baadaye anauzowea na baada ya hapo inakuwa vigumu kuwa na uchamgamfu. Na akijizoweza kuwa na uchangamfu na mazowea ya kueneza uelewa wa dini katika ummah, basi inakuwa sahali kwake kufanya hivo. Kiasi cha kwamba anahuzunika na anahisi dhiki asipofanya jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (27 A)
  • Imechapishwa: 20/05/2021