Wajibu wa mtu wa Bid´ah baada ya kutubu kwa uzushi wake

Swali: Ikiwa kuna mtu amelingania katika upotevu na kuueneza kisha akatubu kwa Allaah, anaadhibiwa kwa madhambi yenye kufanywa na wale waliomfuata?

Jibu: Ni lazima kwake kubainisha na kuweka wazi ya kuwa alikosea na ametubu kwa Allaah juu ya hili. Pengine Allaah akamsamehe. Ama akiwaacha wale waliomfuata na asiwabainishie, ataadhibiwa kwa madhambi yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–09041434.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020